Ukiishi Dar es Salaam jua ni kali sana kiasi kwamba unaweza kudhani Tanzania nzima ina joto la aina hiyo na pengine Tanzania ni kati ya nchi zenye joto zaidi Afrika.
World Population Review wametoa orodha ya nchi zenye joto zaidi duniani na pia kutukumbusha kuwa nchi zilizopo karibu na ikweta ndio zina joto zaidi ya zile zilizopo kaskazini ma kusini mwa mstari wa ikweta.
Miongoni mwa nchi zenye joto zaidi Afrika ni pamoja na ;
Nchi Wastani wa nyuzi joto kwa mwaka (°C)
- Mali 28.25
- Burkina Faso 28.25
- Djibouti 28
- Senegal 27.85
- Mauritania 27.65
Huku Nali ikiongoza kwa kuwa na wastani wa joto kali zaidi duniani, Tanzania ina wastani nyuzi joto 22.35°C kwa mwaka huku Canada ikiongoza kwa kuwa na baridi zaidi ikiwa na wastani wa nyuzi joto -5.35°C
Soma zaidi kuhusu hali ya hewa ya kila nchi.