Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amefafanua kauli aliyoitoa juzi ya kutangaza kutogombea ubunge uchaguzi mkuu 2025 alipokuwa kwenye ibada katika Kanisa la Anglikana Pareshi ya Mtakatifu Michael Kongwa wakati waumini walipokabidhi gari walilonunua kwa ajili ya shughuli za kanisa.
“Sijasema naacha siasa, ila naacha kugombea lakini chama changu kikinituma kazi popote nitakwenda kuifanya hadi hapo Mungu atakapoamua vinginevyo,” alisema Ndugai.
Akifafanua zaidi kuhusu kauli aliyoitoa kanisani, Ndugai alisema haikuwa na tatizo lolote.
“Mimi ni muumini wa hapo, nilimsikia Askofu wangu Chimeledya akisema anataka kupumzika itakapofika mwizi wa nane, ndipo wakati wa kusalimia nami nikasema wakati wangu ukifika siendelei, nataka kupumzika,” alisema Ndugai.