Filamu ya “No Time To Die” inaanza na kwa kumuonesha James Bond na Madeleine Swan wakiwa katika mji wa Matera uliopo kusini mwa nchi ya Italia. Ni muda wa wawili hao kula bata. Matarajio yao ni kuwa hakuna mtu anayewafuatilia kwani wanaishi maisha yao mbali na rada. Hata hivyo, kumbe tayari kuna chui ambaye alikuwa ameshanusa harufu zao. Wakiwa hawajui hili na lile, Bond na Swan wanajikuta ni “target” ya watu ambao wamedhamiria kuwaua.
Wanakimbizwa, wanakoswa koswa na pale njia ya kukimbilia inapokoma, wanajikuta wakiwa wamezingirwa tena na watu ambao bastola zao zimewaelekea na siyo kuwaelekea tu, zinamimina risasi zilizowalenga.
Wanakimbizwa, wanakoswa koswa na pale njia ya kukimbilia inapokoma, wanajikuta wakiwa wamezingirwa tena na watu ambao bastola zao zimewaelekea na siyo kuwaelekea tu, zinamimina risasi zilizowalenga.
Kumbuka hapa tunamuongelea Bond. James Bond na kama umekuwa ukifuatilia filamu za 007, unafahamu aina ya magari anayotembelea. kwa gari la leo, halipitishi risasi lakini haliwezi kubaki hivyo hivyo kwa muda mrefu.
Bond yupo kwenye mawazo mazito akifikiri kama kile kilicho akilini mwake kina usahihi. Mawazo hayo ni kuwa, amesalitiwa na mwanamke ambaye alimpenda. Mwanamke aliyeacha kila kitu kwa ajili yake. Binti Madeleine Swan. Kwa hali aliyopo Bond, hasikii la kuambiwa. Licha ya Swan kujitetea kwa kila hali, Bond anamtelekeza Swan na kuanza kutafuta mwanzo wa uzi ulioagiza kifo chake. Asichokijua ni kuwa, Binti Swan alikuwa mbioni kuitwa mama na mtoto huyo, si wa mwingine bali ni wa Bond.
Silaha zinatengenezwa zinaitwa nanobots ambazo zinaua kwa njia ya maambukizi kama virusi lakini tofauti na virusi ambavyo tumevizoea. Nanobots zinafanya kazi kwa kuua watu ambao vinasaba vyao vimetengenezwa na silaha hizo. Misheni ya Bond ni kumuokoa Obruchev aliyetekwa na magaidi baada ya kutengeneza silaha hizo lakini safari hiyo ni kama kuku kujipeleka kwenye shimo la nyoka wenye njaa kali. Hivyo huenda maisha ya Bond nayo yakawa kwenye hati hati. Kujua nini kinaendelea baada ya hapo tembelea kumbi za filamu kama Century Cinemax na zingine ili uweze kujua mbivu na mbichi za filamu hii ya No Time to Die.