Onyo kwa chama kipya cha Umoja Party

HomeKitaifa

Onyo kwa chama kipya cha Umoja Party

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, amesema ni kosa kisheria kwa chama cha siasa kilichowasilisha maombi ya usajili wa muda kufanya kazi kabla ya kupewa cheti cha usajili.

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza alieleza hayo jana katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyokemea chama cha siasa cha Umoja Party kinachodaiwa kuanza kazi za siasa kabla ya kupewa cheti cha usajili wa muda.

Akinukuu kifungu cha sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 kifungu kidogo cha 7(3) kinachoeleza kuwa “hakuna taasisi itakayofanya kazi kama chama cha siasa hadi kiwe kimesajiliwa kwa mujibu wa sheria.” alieleza Nyahoza.

Huyu ndiye mwanzilishi wa chama kipya cha Umoja

Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba, chama cha siasa cha Umoja Party kimewasilisha maombi ya usajili wa muda na kwa sasa yanafanyiwa kazi hivyo hawakupaswa kuanza kazi kama jinsi wanavyofanya kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha, Nyahoza alisema ni kosa kisheria kutengeneza na kuvaa fulana kwa wanachama na Watanzania wote kwa ujumla na kuwataka kuacha kuzivaa mara moja.

error: Content is protected !!