Spika wa Bunge Mhe. Job Y. Ndugai (Mb), amefanya mabadiliko madogo ya Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni ya 135 (3) – (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Juni 2020. Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:
- Mhe. Godwin Emmanuel Kunambi anahamishwa kutoka kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwenda kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii.
- Mhe. Humphrey Hesron Polepole anahamishwa kutoka Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa kwenda Kamati ya Sheria Ndogo.
- Mhe. Asia Abdulkarim Halamga ameteuliwa kuwa Mjumbe ya Kamati ya Masuala ya UKIMWI.
- Mhe. Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Sheria Ndogo na kamati ya Masuala ya UKIMWI.
- Mhe. Dkt. Medard Matogolo Kalemani ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Sheria Ndogo.
- Mhe. Eng. Dkt. Leonard Madaraka Chamuriho ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Sheria Ndogo; na
- Mhe. Agnes Mathew Marwa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Masuala ya UKIMWI.