Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameguswa na kifo cha muigizaji nguli nchi na mtangazaji Chuma Selemani maarufu kama Bi. Hindu kilichotokea leo majira ya asubuhi akiwa nyumbani kwake Magomeni.
Nimepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kifo cha msanii maarufu wa Kaole, Chuma Selemani maarufu ‘Bi Hindu’. Uweledi wake wa uigizaji na matumizi ya lugha ya Kiswahili yalileta mvuto kwa watazamaji wa Rika zote. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi. Amin. pic.twitter.com/k4aWt7QUey
— Samia Suluhu (@SuluhuSamia) July 9, 2022