Rais Samia ampa miezi mitatu Waziri Aweso

HomeKitaifa

Rais Samia ampa miezi mitatu Waziri Aweso

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa miezi mitatu kwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akamilishe mradi wa maji unojengwa kwa Sh bilioni 1.7 wilayani Monduli.

Alisema jana kuwa serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuchukua maji kutoka mradi wa maji unaotekelezwa jijini Arusha na kuyapeleka Monduli.

Rais Samia aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi eneo la Makuyuni wilayani Monduli wakati akitoka mkoani Manyara na kusema mradi wa Sh bil. 1.7 ni kwa ajili ya kuwapatia maji wananchi wa Mbuyuni, Naiti hadi Losimingori.

Aliagiza mradi wa visima vitatu vilivyochimbwa katika Kitongoji cha Zaburi, visima viwili na kimoja kitongoji cha Meloroni vyenye uwezo wa kutoa maji kiasi cha lita za ujazo milioni 1.1 upatiwe fedha mara moja ili ukamilike Machi mwakani.

 

 

error: Content is protected !!