Rais Samia atoa msamaha kwa wafungwa 4,887

HomeKitaifa

Rais Samia atoa msamaha kwa wafungwa 4,887

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa elfu nne mia nane themanini na saba (4,887) ambapo arobaini na mbili (42) kati yao wanaachiliwa huru tarehe 26 Aprili, 2025 na elfu nne mia nane arobaini na tano (4,845) wanabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huu.

Msamaha huo umetolewa leo wakati Taifa likiadhimisha Miaka 61 ya Muungano wa Tanzania.

error: Content is protected !!