Rais Samia: tudumishe muungani wetu

HomeKitaifa

Rais Samia: tudumishe muungani wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amehutubutia taifa kuhusu miaka 60 ya Muungano huku akisisitiza katika kudumisha uzalendo na mshikamano wa kitaifa.

Katika hotuba hiyo, Rais Samia amewasihi na kuwakumnusha watanzania kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni moja tu ulimwenguni kote hivyo hatuna budi kushikamana na kuulinda muungano huu.

“Jamhuri ya Muungano wa Tanzani ni moja tu ulimwenguni na ndio inayozaa watanzania, Jamhuri hiyo ni yetu na Tanzania ndio kwetu hatuna kwingine katu habadani. Nina wasihi kudumisha uzalendo kwa kuzidisha umoja na mshikamano wakitaifa.” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amewataka wanasiasa kufanya shughuli za kisiasa zinazounganisha watu na kuzingatia misingi ya kisheria.

“Vilevile niwasihi wanasiasa wenzangu kukumbuka kwamba Muungano ni wa watu. Nitoe rai kuwa siasa zetu zijikite katika mafanikio yaliyopatikana katika miaka 60 ya Muungano na tudhamirie kufanya siasa zenye kuleta kuunganisha watu, kuthaminiana na kudumisha misingi ya utawala wa sheria.” amesema Rais Samia.

 

 

 

 

 

 

 

 

error: Content is protected !!