Ramadhani Brothers wameiwakilisha vyema Tanzania

HomeKimataifa

Ramadhani Brothers wameiwakilisha vyema Tanzania

Wanasarakasi wa Kitanzania Ramadhani Brothers, wamefanikiwa kuingia nusu fainali ya mashindano ya Australia Got Talent lakini kushindwa kutwaa ubingwa wa msimu huu wa mwaka 2022.

Mshindi wa mashindano hayo mwaka huu ni kundi la waruka sarakasi wasichana la Acromazing ambao wamejishindia dola za marekani $100,000 sawa na shilingi 233,137,405.55.

Ramadhani Brothers wameonyesha umahiri na ubunifu wa kuruka sarakasi kwa mitindo ya kibbunifu iliyowavutia majaji, watazamaji na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyewapongeza kwa kuiwakilisha Tanzania vyema kwenye mashindano hayo.

Tanzania inajivunia kwa hatua waliyoifikia Ramadhani Brothers kwani huu ni mwanzo mzuri wa safari yao ndefu.

error: Content is protected !!