Sababu ya Mabeyo kuteuliwa na Rais Samia

HomeKitaifa

Sababu ya Mabeyo kuteuliwa na Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA).

Uteuzi huo ulifanyika juzi jioni muda mfupi baada ya kumwapisha Mkuu Mpya wa Majeshi, Jenerali Jacob Mkunda na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Luteni Jenerali Salum Haji Othman.

Uteuzi huo wa Jenerali Mabeyo ni mwendelezo wa serikali kuteua ,aofisa wa juu wa jeshi kushika nyadhifa za mamlaka mbalimbali nyeti za serikali.

Lengo la serikali kuteua maofisa hao wakuu wa jeshi kuwa wenyeviti wa bodi katika mamlaka hizo, inaelezwa na wachambuzi kwamba ni kutokana na nidhamu yao,nia ya kulinda rasilimali za nchi na tabia zao za kiungwana.

Baadhi ya mamlaka zinazoshikwa na maofisa wakuu wa jeshi ni pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) ambayo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ni Meja Jenerali Mstaafu, Hamisi Semfuko na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ambalo Mwenyekiti wa Bodi ni Jenerali mstaafu George Waitara.

 

error: Content is protected !!