Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imekusudia kujenga shule kwenye kila kijiji na vitongoji vikubwa ili kuhakikisha watoto wote wanapata fursa ya elimu.
Akizungumza baada ya kukagua mradi wa Shule ya Msingi Sabasita, Majaliwa amesema ni mkakati wa serikali kuhakikisha kama kuna kijiji kina watu wengi mpango ni kuongeza shule katika eneo hilo.
“Serikali ya awamu ya sita inawapenda watanzania wote ndio maana Rais wetu Dkt. Samia anatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta zote kuanzia ngazi ya Taifa hadi vijijini,” amesema Majaliwa.
Maboresho ya miundombinu ya elimu anayofanya Rais Samia , hasa kwa shule za vijijini yameendelea kutoa hamasa kwa wanafunzi kujifunza zaidi na kuendelea kutimiza ndoto zao.