Simba wasaini bilioni 26.1 na M- Bet

HomeKitaifa

Simba wasaini bilioni 26.1 na M- Bet

Klabu ya Simba ya Dar es Salaam na Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-Bet, leo wametangaza mkataba wao wa udhamini wa miaka mitano wenye thamani ya Sh Bil.26.1.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, akizungumza kwenye mkutano wa kutambulisha mkataba huo leo jijini Dar es Salaam, amesema kampuni hiyo imekidhi mahitaji ya Simba.

“Leo ni siku kubwa kwa Simba na M-Bet. Swali kubwa ni kwa nini M-Bet. Sababu kubwa ni wameweza kukidhi mahitaji yetu.

“Kwa ukubwa wa Simba ni lazima kujihusisha na kampuni ambayo inaongoza kwenye biashara, ambayo wanafanya. Mkiangalia takwimu M-Bet wanaongoza kwa ukubwa Tanzania,” amesema Barbara.

error: Content is protected !!