Steve Nyerere kuvuliwa

HomeBurudani

Steve Nyerere kuvuliwa

Mbunge wa Muhenza ambaye pia ni msanii, Hamisi Mwinjuma maarufu kama Mwana FA amewapa masaa 48 viongozi wa Shirikisho la Muziki Tanzania kuleta jina la msemaji mpya wa Shirikisho hilo kwa kudai kuwa aliyopo sasa Steve Nyerere hajakidhi vigezo na sifa vya kuwa katika nafasi hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wasanii wengine, Mwana FA alisema utaratibu mzuri ufanyike ili aweze kupatikana msemaji mpya wa shirikisho hilo baada ya masaa 48 kuisha.

“Vigezo vya nafasi ambayo mmeitoa inatakiwa kuwa na aina flani ya elimu, inatakiwa kuwa na aina flani ya uzoefu na criteria nyingine ambazo mtu mliyemchagua hana , kwahiyo siis tunachoomba pengine ni ngumu kufanya maamuzi hapa hapa mnataka mkae sasa bodi ikae kweli kwa sababu haikuwahi kukaa tuwape masaa 48 na mtuletee maamuzi ambayo yataturidhisha,” alisema Mwana FA.

Hivi karibuni Steve Nyerere ambaye ni muigizaji alichaguliwa kuwa msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania jambo lilozua mijadala katika mitandao ya kijamii huku wengi wakipinga uchaguzi huo.

error: Content is protected !!