Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na utawala bora, Deogratius Ndejembi ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kufuatilia matumizi ya shilingi trilioni 1.3 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwaajili ya Kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ustawi na Taifa.
Miradi hiyo ya maendeleo inajumuisha ujenzi wa madarasa, Zahanati na vituo vya Afya, Ndejembi amesema kuwa viashiria vya rushwa na uvunjifu wa maadili vimeanza kuonekana kwenye baadhi ya maeneo ambayo fedha hizo zimeelekezwa na Rais Samia kwaajili ya ujenzi wa miundombinu.
Mhe. Ndembeji amefafanua kuwa kuna maeneo imebainika kwamba tofali zinatolewa zaidi ya kilomita 150, jambo ambalo linaongeza gharama za ujenzi lakini pia kuna maeneo gharama ya tofali ni shilingi 1200 lakini wenye nia ovu wanaenda kununua sehemu ambayo linauzwa shilingi 1700.
“Viongozi wanavutana nani apate nini, nani amlete mzabuni wa tofali au saruji na kuna eneo moja mkoani Mara mzabuni huyo huyo kila eneo ”Pesa za ujenzi wa miradi hiyo zilitolewa na shirika la fedha duniani (IMF) kama mkopo kwa ajili ya nchi zilizoathiriwa na janga la Korona.