Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imesema Naibu Waziri wa Ofisi hiyo anayeshughulikia Afya Dk Festo Dugange hajajiuzulu wadhifa huo.
Dugange ambaye yuko akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma baada ya kupata ajali ya gari amekuwa katika vichwa vya habari na mitandao ya kijamii kwa karibu wiki mbili sasa.
Taarifa ya Tamisemi imesema kiongozi huyo hajajiuzulu kama baadhi ya mitandao ya kijamii ambavyo imekuwa ikiripoti.
View this post on Instagram