Baada ya kuibuka kwa malalamiko kuhusu wateja wa mitandao ya simu kununua vifurushi na kupata tofauti na kile walicholipia, Mamlaka ya Mawasiliano kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter umefunguka na kusema kama kuna mteja amekutana na changamoto hiyo basi awasiliane na mamlaka hayo haraka.
TCRA imeona mjadala wa malalamiko kutoka kwa Wadau Mtandaoni kuhusu watoa huduma kubadili bei za vifurushi kimyakimya.
Mamlaka ingependa kuwajulisha kuwa endapo kuna mtumiaji amenunua kifurushi, halafu akapata tofauti na kile alicholipia, awasiliane nasi kupitia 0800008272.— TCRA_TANZANIA (@TCRA_Tz) May 2, 2022
Pia unaweza kuwasiliana na Mamlaka kupitia baruapepe [email protected]. Mamlaka inafuatilia suala hili kwa watoa huduma ili kuweza kubaini ukweli.
— TCRA_TANZANIA (@TCRA_Tz) May 2, 2022