Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA ) leo Mei 9,2022 imeeleza sababu zinazopelekea data kuishia kwa haraka kwenye vifurushi vya watumiaji wa mitandao tofauti nchini.
Hii imekuja baada ya hivi karibuni kuwa na malalamiko kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya simu kuhusu kupanda kwa bei za vifurushi na data kuisha kabla ya wakati unaotarajiwa.
TCRA kupitia kwenye ukurasa wao wa mtandao wa Twitter umeeleza sababu kuu nne zinazopelekea kumalizika kwa hara kwa data.
?Sababu za Data Kuisha Haraka pic.twitter.com/IweDLbcRbH
— TCRA_TANZANIA (@TCRA_Tz) May 9, 2022
Aidha, TCRA imesema bei ya vifurushi vya Data nchini Tanzania ni ya chini kuliko nchi zote za Afrika Mashariki (EAC) na Kusini mwa Africa ( SADC).
?MUHIMU pic.twitter.com/nGLV5zvDLI
— TCRA_TANZANIA (@TCRA_Tz) May 9, 2022