Tozo za miamala zapunguzwa

HomeBiashara

Tozo za miamala zapunguzwa

Taarifa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango inaeleza kwamba Serikali imefanya marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya Kielektroniki za kutuma na kutoa fedha za mwaka 2021 na kupunguza viwango vya tozo za miamala hiyo kwa asilimia 30.

Pia, Serikali imejadiliana na watoa huduma za simu ambao nao wameridhia kupunguza viwango vya tozo wanazotoza katika miamala ya kutoa na kutuma fedha kati ya mtandao na mtandao kwa asilimia 10.

Imeelezwa kwamba viwango vilivyopunguzwa vitawekwa rasmi kwenye tangazo la Serikali la Septemba 1, 2021.

Hii ina maana kwamba viwango vya makato vitapungua kwa asilimia 40.

error: Content is protected !!