Andiko hili fupi la kiteknolojia linakupa mbinu muhimu za kuhakikisha kwamba bando katika simu yako haliishi haraka ili uweze kufanya matumizi yako ya muhimu kwa raha.
Kwa watumiaji wa Android
- Jiunge na Wi-Fi kila unapopata nafasi ya kufanya hivyo
- Jenga tabia ya kutumia huduma za “streaming” kwa kiasi
- Fungua setting
- Nenda kwenye Apps
- Bofya app unayotaka kupunguza matumizi yake ya data
- Bofya mobile data
- Kama sehemu ya matumizi ya data hata kama hutumii app hiyo iko on utaona hii sehemu ya mobile data ina alama nyeupe na bluu. Ili kuzima ibpfye iwe rangi nyeupe pekee.
- Zima automatic updates zisiwe zinafanyika kwa bando la simu bali tu pale unapokuwa sehemu yenye “wi-fi”. Fuata hatua hizi: Nenda katika Settings > iTunes & App Stores > Turn Off Use Cellular / Mobile Data.
- Zima apps zisiwe zinafanya Background Refresh. Hii maana yake apps zitaji-update pale tu unapotaka wewe. Fuata hatua hizi: Settings > General > Background App Refresh > Turn Off au changua baadhi ya apps
- Zima iCloud isifanye kazi wakati unatumia bando la simu. Ifanye tu pale unapokuwa kwenye “Wi-Fi”. Fuata hatua hizi: Settings > Cellular / Mobile Data > Turn Off iCloud Drive
- Zima baadhi ya apps ambazo hutaki zitumie bando bali “Wi-Fi” pekee. Fuata hatua hizi: Settings > Cellular > Chagua apps ambazo hutaki zitumie bando la simu (cellular data).