UJENZI WA VETA WAGUSA MAISHA YA VIBARUA MKINGA

HomeKitaifa

UJENZI WA VETA WAGUSA MAISHA YA VIBARUA MKINGA

Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga ni kati ya maeneo yaliyonufaika na ujenzi wa vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) unaoendelea kufanywa na Serikali ya awamu ya sita katika maeneo mbalimbali nchini.

Chuo cha VETA kinachojengwa katika wilaya ya Mkinga, kitakuwa na madarasa 17 kwa ajili ya kupokea vijana wa Mkinga na maeneo mengine ya Tanzania ili kuwapa ujuzi utakaowezesha kupambana katika soko la ajira au kijiajiri wenyewe.

Kati ya wanufaika wakubwa wa mradi huo unaoendelea wilayani Mkinga, ni wananchi wanaofanya kazi kama vibarua.

Mwanahamisi Jumbe, ni Bibi wa miaka 70 ambaye anafanya kazi mbalimbali katika kukamilisha mradi huo. Anasema anafanya kazi zozote ikiwemo kuchimba mitaro na kufanya usafi.

“Mradi huu umeninufaisha sana, kwa sababu nikipata hela hapa, nikienda nyumbani ninaenda kujiendeleza. Mimi ni mfanyabiashara ndogondogo maandazi na nyinginezo, nikipata hela naenda kujiendeleza zaidi” alisema Mwanahamisi.

Naye Meshack George anayefanya kazi kama fundi msaidizi katika mradi huo, ameishukuru Serikali kwa kuleta mradi huo ambao umemuwezesha kununua shamba na mabati kwa ajili ya kuanza ujenzi wa nyumba yake binafsi.

Vibarua hao wananufaika kutokana na maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassana, kwamba miradi inayojengwa nchini kote itoe kipaumbele kwa wakazi wa maeneo husika, ili wawe wanufaika wakuu wa vibarua hivyo.

error: Content is protected !!