Serikali imesema magari yataanza kulipia fedha yanapopita kwenye Draja la Tanzanite na katika barabara nyingine mbili za haraka za Kibaha-Mlandizi – Chalinze- Morogoro(Expressway)- Tunduma (Expressway) kwa kuwa zote zina sifa za kutozwa fedha.
Hayo yalisema na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, alisema serikali inaendelea kuboresha sekta ya uchukuzi nchini kwa kuendeleza utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara ili kufungua fursa za kiuchumi.
Alisema katika ujenzi huo, Daraja la Tanzanite lililopo maeneo ya Salender, Dar es Salaam lenye urefu wa kilometa 1.03 lililojengwa baharini jirani na ufukwe wa Coco litawekewa malipo ya fedha kwa sababu lina sifa za kufanya hivyo.
Dk Mwigulu alitaja barabara nyingine zitakazowekwa tozo ya barabara kwa sababu zina sifa za kufanywa hivyo ni ile ya Kibaha- Mlandizi- Chalinze – Morogoro ambayo ujenzi wake ukikamilika utakuwa na urefu wa kilometa 158 na Barabara ya Igawa- Songwe- Tunduma ambayo ikikamilika ujenzi wake itakuwa na urefu wa kilometa 218.