Milioni 100 ukimpata huyu mchina

HomeKitaifa

Milioni 100 ukimpata huyu mchina

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam linamtafuta mtuhumiwa, Zheng Lingyao (42) Raia wa China, Mkazi wa Jijini Dar es Salaam Kwa tuhuma kumuua Nannan, (26) Raia wa China, Mfanyabiashara wa Kalenga, Kariakoo.

Wakati huohuo Kampuni anayofanyia kazi mtuhumiwa imetoa zawadi ya milioni 100 kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

Tukio hilo limetokea tarehe 11/06/2022 mtaa wa Kalenga Ilala kwenye ghorofa ya tatu ya wapangaji majira ya saa tano na dakika arobaini na tano usiku ambapo Mtuhumiwa anayetafutwa alifika eneo hilo na kumjeruhi kwa risasi tumboni Nie Mnqin (32) Raia wa China na badaye alimfyatulia risasi FU, Raia wa China ambaye alipoteza maisha.

error: Content is protected !!