Chuo Kikuu cha East Anglia kinafanya majaribio ya wiki 12 ambapo tayari kuna watu maalum wamejitolea kwa ajili ya kufanya majaribio kwenye utafiti huo. Watu hao watatakiwa kwanza kunusa vitu vyenye harufu kali, mbaya na nzuri, kama vile mayai viza au maua yenye harufu nzuri.
Kupoteza uwezo wa kunusa ni moja kati ya dalili kubwa za UVIKO-19, ingawa magonjwa mengine kama vile mafua ya kawaida pia yanaweza kukuleta hali hiyo. Hali ya kupoteza uwezo wa kunusa huondoka baada ya muda, lakini wengine tatizo hilo huwasumbua kwa muda mrefu zaidi.
> Watoto wafanyiwa majaribio ya chanjo ya UVIKO-19
Hali ya kupoteza uwezo wa kunusa sawa sawa huja baada ya tishu laini za kwenye pua kuathiriwa na virusi vya korona. Nchini Ujerumani tayari matumizi ya Vitamini A yameaza kuleta matunda chanya hasa kwa watu wenye tatizo hilo, na Umoja wa Nchi za Kiarabu tayari wameanza utafiti huo kuangalia uwezekano wa Vitamini A kutibu tatizo hilo.
Makundi ya vyakula yenye virutibisho vingi vya Vitamini A ni, karoti, spinachi, pilipili hoho, kunde, mbaazi, choroko, samaki, viazi mbatata, jibini, samli, maboga pamoja na maziwa.
Utafiti ambao unakwenda kutoa majibu kamili bado unaendelea, lakini hadi majibu ya awali yanaoesha kwamba Vitamini A, inaweza kuwa tiba nzuri ya kumaliza tatizo hili.