Vibali vya minara kutoka ndani ya mwezi mmoja na sio miezi 6

HomeKitaifa

Vibali vya minara kutoka ndani ya mwezi mmoja na sio miezi 6

Rais Samia Suluhu Hassan amezitaka mamlaka zinazohusika na utoaji wa vibali vya ujenzi wa minara ya simu kwa kampuni za simu kutoa vibali hivyo ndani ya mwezi mmoja na sio miezi 6 kama ilivyozoeleka.

Amesema hayo kwenye hafla ya utiaji saini Mikataba ya miradi ya kufikisha huduma za mawasiliano ya simu katika kata 763 nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma tarehe 13 Mei,2023.

“Vibali hivi vya minara iliyosainiwa leo visizidi zaidi ya mwezi mmoja vibali vyote viwe vimetoka. Si zaidi ya mwezi mmoja kuanzia leo tarehe 13, 13 mwezi Juni nitamuuliza Waziri mmekwendaje, mmekwama wapi na nani kakwamisha.” amesema Rais Samia.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais Samia alisema kama vibali vitatolewa kwa haraka, huduma za mawasiliano zitawafikia wananchi hasa wale wa vijijini na hivyo kuondoa changamoto ya uwepo wa shida za mawasiliano nchini.

Aidha, Rais Samia amesema kuwepo kwa huduma bora za mawasiliano hususani katika maeneo ya vijijini ni muhimu sana kiuchumi, kisiasa, kijamii lakini hata kiutamaduni lakini hata katika masuala ya ulinzi na usalama wa nchi yetu.

 

error: Content is protected !!