Rick Ross kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro

HomeBurudani

Rick Ross kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro

Rapa wa Marekani William Leonard Roberts II (Rick Ross) leo Machi 31, 2022 katika mahojiano yake na Full Send Podcast ameweka bayana nia yake ya kupanda mlima mrefu kuliko yote Afrika.

‘The roof of Africa’ kama unavyojulikana Mlima Kilimanjaro ni moja ya vivutio vikubwa vya utalii Tanzania na rapa huyo ameweka hadharani mpango wake wa kupanda milima huo na kuwahamasisha na wengine ikiwemo watangazaji Bob Menery wamuunge mkono kwenye hili.

Katika mahojiano yake ya kipindi cha mtandaoni cha ‘Full Send Podcast’ mapema leo, rapa huyo amewaeleza watangazaji wa kipindi hicho, Kyle Forgeard na Bob Menery ameelezea matamanio yake ya kupanda Mlima mrefu zaidi Afrika.

“Mwaka 2024 nitapanda hadi kilele cha Mlima Kilimanjaro,” amesema Rick Ross.

Miezi kadhaa nyuma baada ya mwanamuziki Hamisa Mobetto kurejea kutoka Dubai alipoonekana akiwa karibu na Rick Ross alitaja kuwa rapa huyo wa Marekani anaipenda Tanzania na anategemea kuwekeza hapa nchini na hata kuishi ikiwezekana.

error: Content is protected !!