Huu ni mwezi wa sita wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani kama Rais wa Tanzania. Kwa kipindi chote kama Rais wa Tanzania amepanga na kupangua safu ya uongozi, lengo kubwa likiwa ni kuunda serikali inayohudumia wananchi.
Licha ya kuwa na mwonekano wa upole, kuna viongozi ambao tayari wamekumbana na panga la Rais katika panga/pangua yake serikalini. Wafuatao ni baadhi tu ya viongozi ambao Rais ametengua uteuzi wao kwa nyakati na sababu tofauti tangu aingie madarakani Machi 19 mwaka huu:
1. Faustine Ndugulile
Alikuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
2. Dkt. Medard Kalemani
Alikuwa waziri wa Nishati
3. Lengai Ole Sabaya
Alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai
4. Bakari Msulwa
Alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro
5. Sheila Lukuba
Alikuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Morogoro
6. Albert Chalamila
Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
7. Mhandisi Leonard Chamuriho
Alikuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
8. Thobias Richard
Aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), lakini saa chache baadaye Rais alitengua uteuzi huo.
9. James Mataragio
Alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), lakini saa chache baada ya Rais kutengua uteuzi wake, alimteua na kumrejesha kwenye nafasi hiyo.
10. Profesa Tadeo Andrew Satta
Alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC). Pia Rais alitengua uteuzi wa wajumbe 6 wa bodi ya shirika hilo.
11. Hassan Mwang’ombe
Alikuwa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania
12. Dk Harun Kondo
Alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania
13. Aza Hilal Hamad
Aliteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu. Aliondolewa na na nafasi yake kuchukuliwa na Prisca Joseph Kayombo.
Mbali na kiongozi mmoja mmoja, Rais pia amevunja bodi ya/za taasisi ikiwemo Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania.