Wakutwa na madawa ya kulevya gramu 70.77

HomeKitaifa

Wakutwa na madawa ya kulevya gramu 70.77

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limefanikiwa kumkamata maeneo ya Osunyai, Abdi Hamis (27) mfanyabiashara, mkazi wa Ngarenaro na Ally Said (25) dereva na mkazi wa Olasiti wakiwa wanasafirisha madawa ya kulevya yanayodhaniwa kuwa ni Heroini gramu 70.77 kwa kutumia gari Na. T949DQA aina ya Mercedes Benz zikiwa na tela Na. 253 CXR.

Kamanda Mkuu Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, ACP Masejo amesema Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa watuhumiwa wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo haramu kwa muda mrefu na walikuwa wakifuatiliwa.

“Aidha bado tunaendelea kuwashikilia watuhumiwa hao pamoja na gari hilo na pindi upelelezi utakapokamilik ajalada litapelekwa ofisi ya taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.” alisema Kamanda Masejo.

Kamanda Masejo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi wa watu wanaojihusiha na biashara haramu ya madawa ya kulevya na vitendo vya kiharifu na waharifu ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

 

error: Content is protected !!