Watalii wa kimataifa wamiminika Tanzania kwa ongezeko la 22%

HomeKimataifa

Watalii wa kimataifa wamiminika Tanzania kwa ongezeko la 22%

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia ripoti yake ya mwezi Mei 2024 inaonyesha ukuaji wa sekta ya utalii na namna inavyoendelea kuvunja rekodi kwa ujio wa idadi kubwa ya watalii wa kigeni jambo linalofanya mapato ya sekta hiyo kupaa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watalii wa kimataifa wameongezeka kwa asilimia 21.9 na 21.8 kipindi cha mwezi Machi na Aprili mwaka huu ikilinganishwa na miezi kama hiyo mwaka uliopita.

Kupitia takwimu hizo, Tanzania inakuwa nchi ya kwanza Afrika na ya nne duniani kwa kuwa na ongezeko kubwa la watalii.

Aidha, Sekta ya Utalii imefanya vyema kwenye upande wa mapato ambapo imeingiza jumla ya Dola za Kimarekani bilioni 3.58 na 5.75 kwa mwezi Machi na Aprili mwaka huu kutoka dola bilioni 2.7 na 2.8 kwa mwezi kama hiyo mwaka 2023.

Haya ni matokeo ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu iliyofanya katika kuhakikisha inatangaza vivutio vya kitalii vilivyopo nchini pamoja na kuhakikisha Tanzania inakuwa na amani na utulivi ili watalii wengi zaidi waweze kuja.

Ikumbukwe, juhudi za Serikali zilizoleta ongezeko hilo la watalii ni pamoja na ushiriki wa Rais Samia Suluhu katika filamu ya Tanzania: The Royal Tour na sasa filamu mpya ya “Amazing Tanzania”.

error: Content is protected !!