Katika kikao kilichofanyika usiku wa kuamkia leo Mei 5, Dar es Salaam, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kutafuta njia za kupunguza gharama ya maisha kwa Watanzania katika kipindi hiki cha mfumuko wa bei ya mafuta katika soko la dunia.
Serikali imejikita kutatua tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta Serikali imejikita kutatua tatizo hilo bila kujali kupanda kwa bidhaa hiyo kwenye soko la dunia ili mwananchi asiendelee kuumia, ameeleza Waziri Mkuu.
“Nawaomba Watanzania waendelee kuwa watulivu na waiamini serikali yao. Tunaendelea kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha tunapunguza gharama za maisha kwa wananchi,” amesema.
Wizara ya Nishati tayari inashughulikia kupata njia mbadala za kuagiza mafuta ili kufikia lengo la Rais Samia Suluhu Hassan la kumrahisishia maisha kila Mtanzania
Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati, January Makamba, Makatibu Wakuu, pamoja na watendaji wakuu wa taasisi za EWURA, TPDC na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA).