Wito wa Rais Samia kwa wananchi wa Kakonko

HomeKitaifa

Wito wa Rais Samia kwa wananchi wa Kakonko

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko kuhakikisha wanatunza miundombinu ya afya inayojengwa na serikali ili idumu kwa muda mrefu.

Rais Samia ameyasema hayo leo Oktoba 16, 2022 alipokuwa akizimdua Hospitali ya Wilaya ya Kakonko, Halmashauri ya Wilaya ya Kankoko,mkoani Kigoma iliyojengwa kwa gharama ya Sh bilioni 2.9.

“Wito wangu kwenu ni kutunza mali yenu, hii si mali ya Serikali, jitahidini kutunza hospitali yenu iwahudumie leo, kesho na kesho kutwa,” amesisitiza Rais Samia.

Amesema serikali itaendelea kununua vifaa tiba vya vipimo vyote vinavyohitajika kwa binadamu pale anapotakiwa kuhudumiwa.

error: Content is protected !!