Zawadi za Rais Samia kwa Watanzania kutoka Oman

HomeKimataifa

Zawadi za Rais Samia kwa Watanzania kutoka Oman

Haijapata kutokea, ndivyo unavyoweza kusema kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika suala zima la kukuza uchumi, diplomasia na maendeleo ya kijamii.

Ni siku 467 sasa tangu aingie madarakani, Rais Samia amefanikiwa kuhakikisha serikali anayoiongoza imefanikiwa kuongeza mauzo nje hadi kufikia dola bilioni 10 za Marekani kutoka bilioni saba za awali.

Akizungumzia ziara ya Rais Samia nchini Oman, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus alisema imekuwa na manufaa makubwa ikiwemo ujenzi wa mradi wa bandari ya Bagamoyo ambapo serikali na wawekezaji wote wapo tayari.

Alisema Rais Samia na Mfalme wa Oman, Sultan Haitham Bin Tariq Al Said, wamekubaliana ushirikiano baina ya nchi hizo katika siasa, uchumi na uwekezaji.

Hati za makubaliano zilizofikiwa na wakuu hao wa nchi ni ushirikiano katika sekta ya nishati, elimu ya juu, utalii, uwekezaji ikiwemo ujenzi wa hoteli za nyota tano, kuimarisha makumbusho ya taifa na utafiti maeneo ya historia.

Pia wamekubaliana juu ya uendelezaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na uendelezaji Kanda Maalumu uchumi wa usafiri, lengo ni kuchochea shuguli za kiuchumi zikiwemo bidhaa zinazobebwa na ndege kama nyama, samaki, mbogamboga na matunda.

Faida nyingine ya ziara hiyo

  • Ajira za moja kwa moja kwa watanzania; 
  • Ajira zisizokuwa za moja kwa moja kwa Watanzania na wafanya biashara mbali mbali kupitia mnyororo wa thamani utakaokuwepo
  • Kuongeza kipato kwa Serikali kutokana na kodi mbali mbali zitakazokuwa zinalipwa moja kwa moja Serikalini kutoka kwa wawekezaji.
  • Kuongeza kipato kwa KADCO na hatimaye kuongeza mchango wake kwenye mfuko mkuu wa Serikali ambapo, miradi mbali mbali ya maendeleo kwa wananchi hutekelezwa kwa kutumia mfuko huo.
  • Kusogeza baadhi ya huduma kwa wananchi (maduka na sehemu za burudani) ambazo kwa sasa wanazipata mbali.
  • Kueleza fursa zilizopo Tanzania katika sekta ya nishati na jinsi gani nchi hizi mbili zinaweza kushirikiana.
  • Kuitangaza Tanzania kama kitovu cha nishati kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
  • Tanzania kujifunza kutoka nchi ya Omani jinsi walivyotekeleza mradi wa Gesi ya Kimiminika (Liquefied Natural Gas, LNG) kwa zaidi ya miaka 20.
  • Kutangaza fursa za uwekezaji na ushirikiano katika sekta ya nishati.

Aidha, takwimu zinaonyesha kwamba idadi ya watalii wanaoingia nchini hususani jijini Dar es Salaam imeongezeka kwa asilimia 280 na Arusha asilimia 340 na hii ni kutokana na namna Rais Samia Suluhu anavyojitahidi kunadi utalii na vivutio vilivyopo nchini.

error: Content is protected !!