Zijue njia 7 za kuokoa mafuta

HomeElimu

Zijue njia 7 za kuokoa mafuta

Baada ya bei za mafuta kupanda nchini, watumiaji wengi wa vyombo vya moto wameanza kujiuliza ni namna gani wanaweza kumudu gharama hizo mpya.

ClickHabari tumefanikiwa kuperuzi kwenye tovuti mbalimbali zinazohusika na magari na kukutana na dondoo zitakazomsaidia mwendeshaji wa chombo cha moto kuweza kumudu gharama.

Uzito kwenye buti

Kama wewe umezoea kuweka kila kitu kwenye buti mfano unaenda kijijini na kila unachopewa unaweka kwenye buti, hiyo huongeza matumizi ya mafuta.

Kwa kilo 50 za ziada katika uzani wa kawaida wa gari zinaongeza matumizi ya mafuta kwa asilimia 2, hivyo epuka kuweka vitu vingi kwenye buti.

Upepo wa tairi

Tairi zenye upepo pungufu husababisha upinzani wa mwendo kwenye gari, hii ina maana kwa kila mwendo matairi huzalisha zaidi msuguano kuliko tairi linavyozunguka hivyo inaongeza matumizi ya mafuta kwa asilimia 10.

Breki za ghafla

Kukanyaga mafuta kwa nguvu na kushika breki za ghafla ni jambo la hatari kwa usalama barabarani lakini pia linaongeza matumizi ya mafuta.

Usiendeshe kasi

Spidi rafiki kwa matumizi ya mafuta inayopendekezwa kwa barabara ni kati ya 50 hadi 90 lakini kama unaendesha gari kwa spidi 100, gari yako itapambana na ukinzani wa upepo na kulazimika kutumia mafuta kwa asilimia 15 na kiwango hicho kinaweza kuongezeka endapo spidi itazidi.

Maelezo juu ya kupanda kwa bei za mafuta

Endesha na kiyoyozi 

Unaweza ukashangaa kwani watu wengi wanaamini kwamba kiyoyozi kina maliza sana mafuta ya gari, hali haiko hivyo, kuendesha gari huku vioo vikiwa vimefunguliwa kwa mwendokasi zaidi ya 80km/h husababisha upinzani mwingi wa upepo hivyo gari hutumia mafuta zaidi.

Panga safari kulingana na hali ya foleni

Angalia hali ya foleni kabla ya kuanza safari yako, kama hauna huraka na sio safari ya dharura ni bora kupanga safari yako kwa muda ambao hauna foleni kwani foleni husabbaisha matumizi makubwa ya mafuta.

Kama gari haitumiki izime

Ikiwa kuna kitu kinasubiriwa kwa zaidi ya dakika 3 kabla ya safari ni vyema gari likazimwa na kuwashwa pindi muda wa safari utakapowadia.

 

error: Content is protected !!