Kufuatia kusambaa kwa kasi kwa kirusi kipya cha UVIKO-19 ( Omicron BA.2) duniani, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kirusi hicho hakijafika Tanzania.
Waziri Ummy amesema hayo wakati akipokea chanjo dhidi ya UVIKO – 19 aina ya Sinovac kutoka nchini Uturuki leo, Dar es Salaam.
Kirusi hicho kipya kimezaliwa kutokana na virusi vya UVIKO, Delta na Omicron, hivyo kuitwa “Deltacron”.
Mapema asubuhi ya leo Waziri Ummy amewasiliana na maafisa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu kirusi hicho kipya na kupata taarifa kuwa bado wanaendelea na tafiti kujua makali ya kirusi hicho.
Sampuli zilizochukuliwa kupima endapo Tanzania ina kirusi hicho kipya cha UVIKO – 19 zimeonesha uwepo wa kirusi cha Omicron pekee.Chanjo alizopokea Waziri Ummy Mwalimu leo zitasaidia wananchi kupambana na maafa yanayoweza kusababishwa na virusi vya UVIKO.