Zitto Kabwe amuomba Rais Samia awezeshe kuachiwa kwa Mbowe

HomeKitaifa

Zitto Kabwe amuomba Rais Samia awezeshe kuachiwa kwa Mbowe

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe, amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kusaidia ili ‘mwenzao’ anayekabiliwa na kesi ya jina aachiwe huru.

Akizungumza leo hii wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa siasa unaoendelea jijini Dodoma, Zitto Kabwe alijikita zaidi kwenye kumsihi Rais Samia Suluhu kuunganisha nchi, akisema kwamba kuna mgawanyiko lakini anaamini Rais Samia anaweza kuwaunganisha watu.

Zitto Kabwe alisema, kuna ‘mwenzao’ (wao viongozi wa siasa) hayupo katika mkutano huo kutokana na changamoto za kisheria. Japo Zitto Kabwe hakutaja jina, lakini kiongozi ambaye hajahudhuria mkutanoi huo kwa changamoto za kisheria ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Jambo lingine linaoashiria kwamba ‘mwenzao’ huyo ni Freeman Mbowe, ni ukweli kwamba ACT-Wazalendo walisema moja ya agenda zao muhimu katika mkutano huo ni kushinikiza kuachiwa kwa Freeman Mbowe.

Zitto Kabwe alisema “ “Tuna utamaduni wa kumaliza haya mambo, haitakuwa mara ya kwanza. Tunao wakina Hamad Rashid hapa, wakati umekuwa Waziri kwa mara ya kwanza kule Zanzibar,  ulikutana na mgogoro mkubwa ukazunguka na Muheshimiwa Rais Kikwete sehemu mbalimbali za dunia kwa ajili ya kutatua lile tatizo la mwaka 2001 na watu wote waliokuwa na kesi za jina waliachiwa kwa lengo kwa la kujenga muafaka kule Zanzibar. Tunakuomba sana sana sana, kwa mujibu wa Sheria na kufuata taratibu zote za kisheria, tuasaidie mwenzetu tuwe naye ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja tuunganishe nchi yetu. Tufanye siasa zenye tija kwa maslahi ya nchi yetu”

Mkutano huo unaendelea jijini Dodoma na utarajiwa kufungwa keshokutwa Desemba 17,2021.

 

error: Content is protected !!