Hekta 134 kutengwa kilimo cha bangi

HomeKimataifa

Hekta 134 kutengwa kilimo cha bangi

Nchini Rwanda hekta 134 zimetengwa kwa ajili ya uzalishaji wa zao la bangi baada ya serikali kuanza kutangaza mipango ya kuanza kuzalisha na kusafirisha zao hilo na bidhaa zake kwa ajili ya dawa.

Ni muda mfupi tangu kutolewa uamuzi huo, hatua kadhaa zimechukuliwa kuelekea kuanza kwa shughuli hizo huku Bodi ya Maendeleo ya Rwanda(RDB) ikisema serikali imetenga eneo mahususi la hekta 134 kwa ajii ya uazalishaji wa bangi.

Hata hivyo, hakuna leseni ambazo zimetolewa, kwa kuwa mchakato wa utoaji leseni ni mpana na unahitaji upatanishi na mahitaji ya usalama na miundombinu katika eneo hilo.

Ofisa Mkuu Mtendaji wa RDB, Claire Akamanzi, alisema bangi itakayozalishwa itatumika kwa kuuza nje ya nchi pekee katika masoko makubwa ya Marekani, Canada na Ulaya. 

 

CHANZO: HABARI LEO

error: Content is protected !!