Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imeunga mkono kauli ya Rais Samia Suluhu aliyotoa wakati akihutubia Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mapambano dhidi ya
Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19).
Katibu Mkuu wa EAC, Dkt. Peter Mathuki amesema anaungana na wito wa viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kutaka kuondolewa kwa hakimiliki kwa kuruhusu nchi zaidi hasa zenye kipato cha kati na chini kuzalisha chanjo dhidi ya UVIKO-19.
Akiwa katika mkutano huo nchini Marekani, Dkt. Mathuki alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Balozi Liberata Mulamula, baada ya Rais wa Samia kutoa hotuba yake.
“Ninaunga mkono kabisa maoni ya Rais Suluhu kwamba nchi zinazoendelea lazima zisaidiwe kushughulikia athari za kijamii na kiuchumi za UVIKO-19 ili kufufua ukuaji wa uchumi,” alisema.