Aliyewahi kuwa Waziri wa Utalii na Maliasili, Hamis Kigwangalla amefunguka na kusema kwamba taarifa iliyotolewa na akaunti moja ya mtandao wa Twitter yenye jina la ‘Tanzania Leaks’ kuhusu kukubaliana na matakwa ya katiba mpya.
Leo Jumatatu Mei 9,2022, Mbunge huyo wa Nzega ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akikana taarifa hiyo na kuiomba TCRA kuingilia katika pamoja na kuwachukulia hatua wahusikia wa Tanzania Leaks kwa kile anachodai kutungwa kwa maneno.
Jana @TanzaniaLeaks wameandika uongo. Nakanusha sijasema maneno hayo na wala huo siyo mtazamo wangu. Naomba @TCRA_Tz mchukue hatua stahiki dhidi yao. Mimi nipo likizo ya kuongea na vyombo vya habari na mitandaoni si-post chochote, bungeni sijaongea, wametoa wapi maneno hayo?
— Dr. Hamisi Kigwangalla (@HKigwangalla) May 9, 2022