Nelson Mandela kufundisha kwa njia ya masafa

HomeKitaifa

Nelson Mandela kufundisha kwa njia ya masafa

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Saynasi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Profesa Emmanuel Luoga amesema taasisi hiyo imejipanga kuja na mfumo wa ufundishaji kwa njia ya masafa.

Profesa Luoga aliyasema hayo wakati wa kuelezea utekelezaji wa mradi wa kipaumbele wa kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambao utatumia sehemu ya mkopo wa dola za Marekani milioni 10 ambazo ni mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia.

Alisema katika mradi huo taasisi itaimarisha mifumo ya Teknolojia kwa kuboresha ufundishaji kwa njia ya masafa (e-learning).

“Kwenye vyuo vingi, shule za sekondari na msingi kuna malalamiko walimu hawatoshi hasa walimu wa Hesabu, kwenye e-learning anaweza kuwa mwalimu mmoja akafundisha hata madarasa 10,” alisema Profesa Luoga.

Aidha, Profesa Luoga alisema pia kiwango cha fedha hizo za mkopo kitatumika katika kuhakikisha taasisi inapata ithibati ya maabara ili kufikia viwango vya kimataifa.

 

error: Content is protected !!