Rais Samia afanya mazungumzo na viongozi wa TEC

HomeKitaifa

Rais Samia afanya mazungumzo na viongozi wa TEC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), katika hatua inayolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na viongozi wa dini.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Ikulu ya Chamwino, Dodoma, yakijikita katika masuala mbalimbali ya kitaifa yanayogusa jamii, ikiwemo kisa, imani na maendeleo, pamoja na umuhimu wa kuimarisha amani, mshikamano na kujenga mustakabali mwema wa Taifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, mazungumzo hayo pia yameangazia nafasi ya madhehebu ya dini na viongozi wa dini katika kujenga jamii yenye maadili mema, uwajibikaji na mshikamano, pamoja na mchango wao katika ustawi na maendeleo endelevu ya Tanzania.

Rais Samia amewashukuru viongozi wa TEC kwa kukutana na kujadiliana naye masuala yenye tija kwa Taifa, akiahidi kuendelea na utamaduni wa kushirikiana na kushauriana na viongozi wa dini na makundi mbalimbali ya jamii kuhusu masuala muhimu ya kitaifa.

error: Content is protected !!