Chama cha Wanasheria Tannganyika (TLS) kimependekeza uwekwe utaratibu unaozuia watumishi wa umaa kusimamia uchaguzi pamoja na kuwepo kwa utaratibu wa kisheria kwa ajili ya kuviwezesha vyama vya siasa kufanya mikutano yao kwa uhuru na kutaka kuondolewa utaratibu wa Jeshi la Polisi kuzuia kufanyika kwa mikutano hiyo.
Akiongolea pendekezo hilo, Meneja wa Miradi wa TLS, Mackphason Buberwa alisema uchaguzi ni suala la kuaminiana hivyo inapotokea mtumishi wa umma kupewa nafasi ya kwenda kusimamia uchaguzi wa kisiasa huenda ikaleta upendeleo kwa chama kimojawapo.
“Inapotokea msimamizi huyu kuwa mtumishi wa umma, na bosi wake anagombea katika eneo ambalo yeye ameteuliwa kusimamia uchaguzi huo hawezi kutenda haki hivyo hili tumependekeza litazamwe,” alisema Buberwa.
Pia, Buberwa alisema zuio la mikutano linapaswa kuwa limetoka mahakamani na hata inapotolewa mahakamani lisichukue siku nyingi tangu siku ambayo chama hicho kimepanga kufanya mkutano.