Vita ya Urusi-Ukraine ilivyoathiri bei za mafuta

HomeBiashara

Vita ya Urusi-Ukraine ilivyoathiri bei za mafuta

Kupanda kwa bei ya mafuta kumewaacha wamiliki wa vyombo vya moto, madereva daladala hata watembea kwa miguu kutaharuki pasi na kujua kuwa Tanzania si waathirika pekee bali bei zimepanda kwa ujumla kwenye soko la dunia.

Urusi ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mafuta ghafi duniani akishika nafasi ya pili kwa kuzalisha zaidi ya lita milioni 10.8. Kwa sasa Marekani inashika nafasi ya kwanza kwa kuzalisha zaidi ya lita milioni 12.1 na Saudi Arabia wanaoshika namba tatu wakizalisha lita milioni 9.5 za mafuta ghafi kwa siku.

Kutokana na vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine, vizuizi vingi viliwekwa kwa Urusi ikiwemo vyanzo vyake vya mapato na hivyo kulazimika kwa nchi mbalimbali kugoma kuendeleza biashara na Urusi kwa kipindi hiki.

Marekani imetaka kuweka kikwazo kwenye ununuzi wa mafuta kutoka Urusi na kusema kwa sasa usambazwaji wa mafuta uelekezwe kwenye nchi nyingine hoja inayokataliwa na viongozi wa Ulaya.

Maelezo juu ya kupanda kwa bei za mafuta

Kuwepo kwa vita peke yake kunapunguza nguvu ya uzalishaji wa mafuta Urusi hivyo kumaanisha kuwa kiwango cha mafuta kwenye soko la dunia kinashuka kutokana na uhaba wa mafuta na pia upatikanaji wake si rahisi tena kama ilivyokuwa mwanzo hivyo kufanya bei kupanda zaidi ya ilivyotegemewa.

Huku kukiwa na vikwazo vya kibiashara kimataifa kwa Urusi ni dhahiri kwamba hata kwa vile vichache walivyobaki navyo kwaajili ya biashara watajitahidi kuuza kwa bei ya juu ili kufidia pesa waliyokosa kwenye vyanzo vingine vya mapato.

Pipa (barrel) moja la mafuta ghafi kwa sasa linauzwa kwa takribani dola $140 sawa na takribani laki tatu, ishirini na tano elfu. Huku matumizi ya mafuta kwa Tanzania ni takribani pipa 35,000 za mafuta safi kwa siku. Zaidi ya pipa milioni mbili na nusu (2,500,000) kwa mwezi sawa na takribani lita milioni 400 za mafuta.

Barrel 1 = lita 158.987.

Miongoni mwa nchi 20 zinazoongoza kwa uzalishaji wa mafuta zipo nchi za Afrika zikiongozwa na Nigeria lita milioni 1.9 , Angola lita milioni 1.2, Libya lita milioni 1.07 na Algeria lita milioni 1.03.

Zijue njia 7 za kuokoa mafuta

Waathirika wa kupanda kwa bei ya mafuta ambao ni wamiliki wa vyombo vya moto hadi bei za usafiri wa kukodi si Watanzania pekee, bali dunia kwa ujumla.

Hakuna anayejua lini vita hii itaisha hivyo kila mmoja anajitahidi kuhakikisha shehena aliyonayo inadumu kwa muda mrefu lakini pia kuweza kumudu kununua mafuta kwa bei hiyo mpya kwenye soko la dunia bila kuathiri uchumi wa sekta nyingine.

Chanzo: Investopedia, world population review.

error: Content is protected !!