Watu wanne, wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia baada ya basi la Kampuni ya Miza Express lililokuwa likitokea Mpanda kuelekea Bariadi kuacha njia na kutumbukia bondeni katika eneo la Kijiji cha Ngukumo, Wilaya ya Nzega mkoani Tabora majira ya saa 9 usiku.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Twawa Lulengelule, waliofariki ni wanaume watatu na mwanamke mmoja.


