Waziri Mkuu atoa msimamo kuhusu Ngorongoro

HomeKitaifa

Waziri Mkuu atoa msimamo kuhusu Ngorongoro

Waziri MKuu, Kassim Majaliwa amesema serikali inaangalia utaratibu utakaofaa kuhusu suala la uhifadhi katika eneo la Loliondo lililopo kwenye Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.

“Katika mjadala wetu wa leo, mmetoa maoni nasi tumeyapokea. Bado Serikali inayaangalia maslahi mapana ya umma. Tutawashirikisha pia ni lipi linamaslahi mapana kwa watanzania,” alisema Majaliwa.

Majaliwa alisema hayo wakati akizungumza na wadau wa uhifadhi kwenye kikao kilichofanyika Wasso-Loliondo na kueleza kwamba alichoenda kufanya ni utejelezaji wa ushairi uliotolewa na wabunge kwa serikali kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili na Utalii iliyoilekeza serikali iende katika maeneo ya Loliondo, Ngorongoro na Sale na kuzungumza na wananchi.

“Kama ambavyo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza lazima tuimarishe utalii na kuhakikisha wananchi wanashirikishwa. Waheshimiwa wabunge ambao ndio wawakilishi wametoa maoni yao ikiwemo kushauri suala la ushrikishwaji na ndio maana leo nimekuja hapa kuwasikiliza,” alisema Majaliwa.

Aidha, wadau hao pia waliomba wapatiwe elimu ya uzazi wa mpango, wapimiwe ardhi za vijiji ili kupunguza migogoro inayojitokeza mara kwa mara.

 

error: Content is protected !!