Miaka 5 jela kwa kutumia mualama uliokosewa

HomeElimu

Miaka 5 jela kwa kutumia mualama uliokosewa

Maskini akipata, matako hulia mbwata ndio msemo unaoweza kufananishwa na kile alichofanya Sibongile Mani, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Walter Sisulu (WSU).

Mnamo Juni Mosi, 2017, Sibongile Mani (31) alipokea kiasi cha R14 m kutoka bodi ya mkopo wa elimu ya juu ya Afrika Kusini (NSFAS) sawa na takribani TZS 2.23bn kwenye akaunti yake badala ya kupokea R1398 ~ TZS 222,816 kwa mwezi huo kama ilivyopaswa.

Akiwa tu ni mwanafunzi wa uhasibu mwaka wa pili kipindi hicho, Mani alianza matumizi ya pesa hizo pasi na kuwasiliana na NSFAS kwa siku 73 huku akikadiriwa kutumia takribani milioni mbili kwa siku.

Kabla ya NSFAS kutambua kosa hilo Agosti 13 mwaka huo, Mani alikuwa akinunua nguo za kila aina, na pochi kila siku.

Baadhi ya wanafunzi wenzake walianza kuona mabadiliko katika mtindo wa maisha wa Mani, kwani alianza kununua nywele za gharama, iPhone mpya na ghafla akaanza kutumia pombe za gharama, jambo lililowashitua wengi wao.

Mambo muhimu ya kufahamu kabla ya kuanza kulipa mkopo wa chuo

Jaji Twanette Olivier amemkuta Mani na hatia na kumhukumu miaka 5 jela kwa wizi wa fedha za NSFAS bila ya kuwa na wasiwasi wala kujali kuwa kuna wanafunzi wengine wamekosa pesa kutokana na tamaa zake.

Ameeleza kuwa pengine ingekuwa hukumu ya tofauti kama pesa hizo zingetumika tofauti huku akisema pesa hiyo”haijatumiwa kwa vitu muhimu… iliongozwa na uchoyo, sio uhitaji.”

“Wewe, na nafsi yako, mlifanya uamuzi mnamo Juni 1, 2017, na mlifanya hivyo mara kwa mara kwa siku 73 mfululizo, mara kadhaa kwa siku,”Jaji Olivier alimweleza Mani.

Kampuni iliyokosea muamala ililazimika kuzilipa pesa hizo ili kusudi wanafunzi wengine 585 waweze kupata pesa ya kujikimu katika masomo yao.

Jela miaka 60 baada ya kumbaka mama miaka 56

Ndani ya saa mbili baada ya kupokea pesa hizo, Mani alitumia takribani shilingi milioni 3.2 ‘dryer’ la nywele, vifaa vya kunyooshea nywele, na vifaa  vya jikoni vya bei ya juu ikiwemo mashine ya kukaanga vyakula bila mafuta (airdryer). Ndani ya siku 73 tangu apokee pesa hiyo Mani alitumia tayari milioni 130.4.

Mahakama imesema haiwezi kubadili hukumu kwa kuwa watu wanasema Mani anatoka kwenye maisha duni, kwani hayo ndiyo maisha ya Waafrika Kusini walio wengi na hivyo haifanyi kitendo chake kuwa sawa.

Sibongile Mani ni mama wa watoto wawili wadogo.

error: Content is protected !!